WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema
wanajeshi 6,000 wataondoka uraiani na kurudi kambini mwaka huu baada ya
nyumba zao kukamilika.
Aidha, wizara hiyo inaweka alama katika maeneo yote ya jeshi ili
kuondoa migogoro na wananchi na kuwalipa fidia wote waliovamia maeneo
hayo ili waondoke.
Dk Mwinyi alisema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha
Tunatekeleza, kinachoandaliwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na Kituo cha
Televisheni cha Taifa cha TBC1.
Dk Mwinyi alisema kwa sasa wameingia mkataba na kampuni, inayojenga
nyumba kwa ajili ya makazi ya wanajeshi 10,000 na utekelezaji wa nyumba
6,000 umeanza na zinakaribia kukamilika.
Alisema lengo ni kujenga nyumba hizo nchi nzima katika kila eneo
lenye kambi, lakini awamu ya kwanza imechukua baadhi ya mikoa kwa
kujenga nyumba 6,000 na baadhi ya mikoa itakuwa awamu ya pili nyumba
4,000.
“Kwa awamu ya kwanza nyumba hizo zitakamilika mwaka huu na awamu ya
pili tunategemea kuanza mchakato na tunategemea kukamilisha mapema
iwezekanavyo lakini itategemea na mazungumzo,” alisema.
Kuhusu migogoro ya wanajeshi na wananchi, alisema inatokea kutokana
na awali jeshi lilikuwa likipewa maeneo bila hati, lakini baada ya ardhi
kuwa na thamani kumekuwa na ongezeko la watu wanaoingia katika maeneo
hayo na kuzua migogoro.
Dk Mwinyi alisema kipaumbele katika bajeti ya mwaka huu ni jeshi
kupata zana na vifaa wanavyohitaji kwa majeshi yote na wameingia
mikataba na zana hizo zitaanza kuingizwa nchini na kulipa kwa miaka
mitano mpaka saba wakati vifaa vinavyohitajika vimeishapokelewa.
Home
News
Slider
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Hussein Mwinyi asema wanajeshi 6,000 wataondolewa uraiani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment