Image
Image

14 wafariki,36 wajeruhiwa kwenye mashambulizi ya silaha, mjini Kabul

Watu 14 akiwemo afisa mmoja wa polisi wameripotiwa kuuawa kwenye mashambulizi ya silaha yaliyotekelezwa kwenye hafla ya maombolezo iliyokuwa ikifanyika katika eneo la makaburi ya mashujaa lililoko mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan.Watu wengine 36 pia wameripotiwa kujeruhiwa vibaya kwenye mashambulizi hayo yaliyoendeshwa katika eneo kubwa la makaburi ya Kishia la Karte-i Sakhi.
Idadi ya vifo inahofiwa kuongezeka kutokana na hali mbaya za majeruhi.
Mshambuliaji aliweza kuangamizwa baada ya muda mrefu wa makabiliano katika eneo la tukio.
Kundi la Taliban limetoa maelezo na kutangaza kutohusika na mashambulizi hayo.
Mnamo mwezi Julai, shambulizi la kujito mhanga liliwahi kutekelezwa wakati wa maandamano ya wafuasi wa Shia na kusababisha vifo vya watu 80 na majeruhi 200.
Baadaye kundi la DAESH lilitoa maelezo na kutangaza kuhusika na utekelezaji wa shambulizi hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment