MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekiri kuwapo
uhaba wa dawa na vifaa tiba katika hospitali za Serikali nchini.
Amesema uhaba huo wa dawa ni changamoto ya muda
mfupi na Serikali inatafuta ufumbuzi wa haraka kuwahudumia wananchi.
Alikuwa akizungumza Dar es Salaam jana wakati
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya kina mama na watoto katika
hospitali zote za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam.
Samia alisema anatambua changamoto zinazoikabili
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba ni ukosefu
wa dawa.
“Natambua katika hospitali zetu za rufaa tuna
changamoto ya vifaa tiba na dawa, lakini Serikali tunaifanyia kazi kila
mwananchi aweze kupata huduma hizo kama ilivyopangwa,”alisema.
Alisema idadi watu wanaoongezeka katika
Mkoa wa Dar es Salaam husababisha msongamano wa wajawazito na watoto katika
hospitali za Serikali na kuwafanya kina mama walale chini au walale mbali na
watoto wao.
“Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, takriban
wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000, hufa kila mwaka kutokana na uzazi na
asilimia 80 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, umbali wa
vituo vya afya, upasuaji wa huduma za dharura ya upasuaji kwa wajawazito na
kuongezewa damu.
“Kwa Mkoa wa Dar es Salaam peke yake, kuna zaidi ya
hospitali 42 zinazotoa huduma za dharura za uzazi kwa kasi ya ukuaji wa jiji na
bado Serikali inahitaji zaidi ya hospitali 30 ndani ya miaka 10 ijayo,”
alisema.
Kwa mujibu wa Samia, mradi wa ujenzi huo utagharimu
Sh bilioni 4.5 kwa hospitali tatu na kila hospitali yenye ghorofa tatu na
uwezo wa kuwekwa vitanda 150, itagharimu Sh bilioni 1.2.
Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha hospitali
zote za rufaa zinaendelea kuimarishwa ili kutoa huduma bora za afya ikiwamo
afya ya mama na mtoto.
.........................................................................................................................................................Kwa ufupi kauli ya waziri wa Afya Ummy Mwalimu juu ya uhaba wa dawa nchini ilikuwa hivi.
10 October 2016 Serikali imekanusha taarifa zilizoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi pamoja na mitandao ya kijami kwamba bohari kuu ya dawa na vituo kadhaa vya afya nchini vinakabiliwa na uhaba wa dawa nakusema kuwa taarifa hizo si sahihi na zinalenga kupotosha umma na kuwatia wasiwasi usio wa lazima wananchi.
“Dawa zote muhimu kwa binadamu zinapatikana kwenye bohari kuu ya dawa kwa masaa 24 kinyume na watu na Taasisi zisizo za kiserikali kusambaza maneno kuwa MSD imeishiwa dawa kitendo ambacho sio cha kweli dawa zipo na zinasambazwa kwenye vituo vyote vya afya” Alisema Mhe. Ummy.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambapo amesema kwamba
hali ya dawa nchini ni nzuri kutokana na dawa zote muhimu kuwepo katika maghala
ya dawa huku dawa nyingine zikiendelea kupatikana kwa kuagizwa kutoka
sehemu mbalimbali nchini.
Aidha Ummy amesema kuwa ili kutekeleza
mpango wa sera ya afya ya Serikali ya tano ,jumla ya shilingi bilioni
251 zimetengwa ili kuweza kuhakikisha dawa za binadamu zinapatikana kila wakati pindi zinapohitajika kutoka MSD ili kutoa huduma bora kwa watanzania.
Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania.
Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2, chanjo za Pepopunda dozi milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.
“Tulikuwa na tatizo la chanjo kama wiki nne zilizopita lakini Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania.
Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2, chanjo za Pepopunda dozi milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.
tumejitahidi na tumeweza kuleta chanjo zote muhimu pamoja na kuagiza
chanjo za surua ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuhakikisha
chanjo zinapatikana kwa wingi nchini” alisisitiza Waziri huyo.
Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kununua na kufanya uzalishaji wa dawa katika viwanda vya ndani ili kuweza kuchangia uchumi wa viwanda vya ndani ili tufikie uchumi wa kati.
Waziri Ummy aliwataka Wakurugenzi wa Vituo vya Afya pamoja na Waratibu wa Afya wa Wilaya kuagiza dawa MSD mapema bila ya kusubiri ziishe kabisa kwenye vituo vyao ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment