Image
Image

Ombi la kutafuta hifadhi kwa wahaini 4 wa jaribio la mapinduzi lakataliwa nchini Ugiriki

Wahaini 4 kati ya 8 wa kundi la FETO walioshiriki kwenye jaribio la mapinduzi ya Julai 15 na kutorokea Ugiriki wamewasilisha ombi la kutafuta hifadhi nchini humo.Kamati inayohusika na suala la hifadhi nchini humo imeripotiwa kukakaa ombi la wahaini hao 4 waliotaka kupewa hifadhi kwa misingi ya vitisho vya kisiasa.
Kufuatia uamuzi huo, idadi ya wahaini waliokataliwa kupewa hifadhi nchini Ugiriki imefikia 7.
Mmoja wa wahaini hao naye anaarifiwa kusisitiza kamati ya hifadhi izingatie ombi lake.
Baada ya kufeli kwa jaribio la mapinduzi ya Julai 15, wahaini 8 walitorokea Dedeağaç nchini Ugiriki kwa kutumia helikopta ya kijeshi aina ya Sikorksy na kuanza kuomba hifadhi baada ya kutua.
Tangu siku hiyo baada ya kukamatwa kwao, wahaini hao wamekuwa wakizuiwa chini ya ulinzi katika gereza la Athens.
Kwa upande wa Uturuki, serikali imekuwa ikisisitiza kurudishwa kwa wahaini hao wanaokabiliwa na kesi 4 zinazohusu jaribio la mapinduzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment