Na.Immaculate Makilika – MAELEZO.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari– MAELEZO Bw. Hassan Abbas amesema kuwa waandishi wa
habari hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu muswada wa huduma za habari kwa
vile hakuna mwandishi wa habari atakayefukuzwa au kuachishwa kazi kwa
kigezo cha kutokuwa na elimu katika ngazi ya shahada ya kwanza.
Akizungumza katika kipindi cha mahojiano cha Clouds360 kinachorushwa na kituo cha
televisheni
cha Clouds, Bw. Abbas amesema hakuna haja ya waandishi wa habari
kuuhofia muswada huu badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni
yao ili
kuuboresha zaidi.
“Sheria itatoa kipindi cha miaka 5 ili watu wajiendeleze katika taaluma hii ya habari,
hivyo hakuna mwandishi wa habari atakayefukuzwa au kusimamishwa kazi kwasababu
ya huu muswada kwa vile lengo ni kuwaandaa waandishi ili waweze kufanya kazi vizuri
kwa kuzingatia taaluma”alisema Bw. Abbas
Bw. Abbas aliongeza kuwa kigezo cha taaluma kwa wandishi wa habari hakitaainishwa
katika sheria bali katika kanuni.
Aidha
Bw.Abbas ameongeza kuwa katika historia ya masuala ya habari nchini huu
ni muswada pekee unaolenga kulinda wanahabari kwani unazungumzia hali
halisi ya mwandishi wa habari, ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya
mwaka 1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari pekee.
Muswada
wa huduma za habari umetokana na maoni ya wadau baada ya kuona mapungufu
katika sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ilitungwa wakati ambapo
hakukua na maendeleo makubwa katika sekta ya habarinchini.
Aidha,wadau
na waandishi wa habari pamoja nchini wameombwa kuendelea kutoa maoni
yao kwa kutuma barua pepe kupitia anuani ya cna@bunge.go.tz ilikutoa
fursa ya kuboresha muswada huo kabla ya kuwa sheria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment