ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, ameshtushwa na baadhi ya watu
walioibukaa na kujiita walimu na manabii huku dhamira yao ikiwa ni
kuwatapeli wananchi.
Kutokana na hali hiyo Askofu huyo amewaonya waumini kuwa macho ili
kuwaepuka watu hao kwani nia yao si njema kwao na taifa kwa ujumla.
Askofu Shao alisema hayo juzi katika ibada maalumu ya uzinduzi wa
jengo la Kanisa la Mtaa wa Kimala, Usharika wa Mwangaria, uliopo kata ya
Kahe, wilayani Moshi.
Alisema kumekuwa wimbi kubwa la kuibuka kwa madhehebu mbalimbali ya
dini nchini na kuongozwa na watu wanaojiita manabii na walimu huku nia
yao ikiwa ni kujipatia fedha na si kueneza neno la Mungu kama
inavyodhaniwa.
“Watu hao ambao wamekuwa wakijipambanua kuwa wametumwa na Mungu,
wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo la kujitafutia fedha za kujikimu
katika maisha yao, huku wakipotosha ukweli kuhusu neno la Mungu jambo
ambalo ni hatari.
“Nawaomba waumini kusimamia imani zenu ili kuepuka kuyumbishwa
kiimani na baadhi ya walimu na manabii wa uongo wenye kujali maslahi yao
binafsi badala ya ukweli wa Mungu,” alisema.
Awali kiongozi wa usharika huo, Mchungaji Richard Njau, alisema mradi
wa ujenzi wa kanisa hilo umegharimu zaidi ya Sh milioni 58 hadi
kukamilika kwake ambapo awali kabla ya kukamilika kwa ujenzi huo waumini
walikuwa wakisali na kuabudu chini ya miti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment