MTU mmoja Mkenya ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kumchoma kisu
askari aliyekuwa akilinda ubalozi wa Marekani jijini Nairobi nchini
Kenya.
Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Girigiri katika jijini la Nairobi
Vitalis Otieno amesema polisi wamemuua mtu huyo na kwamba, jina lake
halitatolewa wakati tukio bado liko wenye uchunguzi.
Amesema lengo la mtu huyo kumshambulia askari bado halijajulikana. Askari alichomwa kisu kichwani.
"Askari alijibu shambulio kujilinda na amefanikiwa kumuua
mshambuliaji. Ofisa wangu amelazwa hospitali katika hali imara. Mtu huyo
amekufa papo hapo," alisema Otioano.
Taarifa zaidi kuhusu majeraha aliyepata askari huyo hazijafahamika.
Ubalozi wa Marekani umethibitisha kuwa mtu huyo ameuawa nje ya eneo
lake na kwamba hakuna mfanyakazi wa ubalozi aliyehusika katika tukio
hilo.
Ubalozi wa Marekani uko wilaya ya Girigiri katika jiji la Nairobi ukiwa miongoni mwa balozi kadhaa na ofisi za Umoja wa Mataifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment