Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo
ameondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali
ya siku mbili nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe.
Uhuru Kenyatta.Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na viongozi
mbalimbali wa serikali akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es
salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama.
Mara baada ya kuwasili nchini Kenya, Rais Magufuli atafanya
mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, na baadaye
atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati
Mzee Jomo Kenyatta.
Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji
wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa
Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria
dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
Ikulu Jijini Nairobi
Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa
kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini
Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern
By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Barabara hiyo mchepuko ya Southern
By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya,
inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na
chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika
Jiji hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment