Image
Image

Baada ya Mjane kulazimishwa kuuza nyumba yake Tegeta, DC Kinondoni aingilia kati na kutoa maagizo.

Dar es Salaam.
Ikiwa ni siku moja kituo cha Habari cha ITV kurusha habari ya Mjane Bi. Habiba Mustapha mwenye umri wa zaidi ya miaka 60 mkazi wa eneo la Tegeta kwa ndevu jijini Dar es Salaam kuiomba serikali kuingilia kati mgogoro kati yake na Bwana Emir Oiso Reshea ambaye amekuwa akimng'ang"aniza mjane huyo amuuuzie nyumba yake na kwamba kushindwa kumuuzia nyumba hiyo ataivunja kwa lazima, hatimaye Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi ameingilia kati suala hilo.
Mapema leo 10 Octoba 2016 asubuhi na mapema mkuu huyo wa wilaya amepiga kambi eneo hilo la Tegeta kwa ndevu na kusalimiana na wananchi huku akielekeza mawazo yake kwa mjane anayetaka kudhulumiwa nyumba yake na tajiri ambaye amekuwa akitumia mbinu nyingi tu za kutaka kununua nyumba ya kikongwe huyo kwa nguvu, ambapo sasa amediriki kuingia ndani ya kiwanja cha bibi huyo na kuamua kuchimba shimo hatua chache kutoka mlango wa nyumba ya bibi huyo, huku mjumbe wa mtaa huo akisema juhudi zao za kumsaidia bibi huyo zimekuwa zikikatishwa  tamaa.
Mku huyo wa wilaya Hapi leo ameongozana na wataalamu wa mipango miji, muhandisi wa manispaa na askari wa jeshi la polisi na kuagiza kuvunjwa kwa ukuta ulioziba njia za wananchi kupita, kufukiwa kwa shimo lililochimbwa kabla ya saa 12 jioni leo na kumtaka OCD Kawe kuchunguza tuhuma za mfanyabiashara huyo kudaiwa kusema kuwa
"serikali iko mfukoni mwake" na ikibainika kuwa ni kweli akamatwe mara moja na kuhojiwa na vyombo vya dola.
Wataalamu wa makazi na mazingira wa manispaa ya Kinondoni wamesema mfanyabiashara huyo atazuiwa kuendelea na ujenzi na wamemtaka kuwasiliha nyaraka zake zote katika ofisi za manispaa.
Kwa upande wa wakazi wa eneo hilo hawakuweza kuficha hisia zao kwa kile wanacho kiona ambapo wamesema kuwa tajiri huyo amekuwa  akiwalazimisha wakazi wengi kununua nyumba zao kwa nguvu,ambapo lengo lake ni kununu nyumba za eneo hilo zote.
Tajiri huyo tulimtafuta kwa njia ya simu kuhusu tuhuma hizo ambapo alidai kwamba yuko moshi mkoani Kilimanjaro  na alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alikanusha kutumia nguvu ya fedha kuwang'ang'aniza wakazi wa maeneo hayo wamuuzie nyumba zao.
Video ya mjane akiomba msaada baada ya kurushwa na ITV 9 Octoba 2016 hii hapa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment