Rais
wa Colombia Juan Manuel Santos amesema kuwa atatoa pesa kutoka katika
tuzo yake ya amani ya Nobel ili kuwasaidia waathirika wa mgogoro katika
nchi yake. Alipata tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za makubaliano ya
amani na kundi la kigaidi la FARC.
Santos na kiongozi wa kundi hilo
Timochenko walisaini makubaliano ya amani mwezi uliopita ili kumaliza
mgogoro wa zaidi ya miongo miwili.
Lakini wananchi wa Colombia
walipiga kura ya hapana juu ya makubaliano hayo. Santos anatarajia
kupokea zaidi ya dola mia tisa elfu kutoka kamati ya Nobel.
Home
Kimataifa
Slider
Rais wa Colombia kutoa tuzo yake ya amani ya Nobel ili kuwasaidia waathirika wa mgogoro.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment