Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar.
SERIKALI ya
Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha
kwamba Hospitali na Vituo vyote vya afya vinapatiwa dawa zote muhimu kwa
ajili ya wananchi.
Mkurugenzi
wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamada amesema Serikali
tayari imeidhinisha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kununulia dawa na
Wizara imeshatumia shilingi milioni 600 kununua dawa ambazo zitatosha
katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Amesema
katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shilingi bilioni tano
kwa ajili ya kununulia dawa ambazo zinakidhi mahitaji ya wananchi
katika kuendeleza azma ya Serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi
bila malipo.
“Hakuna haja
ya kuweka akiba dawa wapeni wananchi, dawa zipo zakutosha na utaratibu
wa kuagiza nyengine umeshaanza, ”alisisitiza Mkurugenzi wa Bohari Kuu.
Daktari
Msaidizi wa Hospitali ya Makunduchi Dkt. Asha Salum Hassan amesema
hali ya dawa hivi sasa inaridhisha na dawa nyingi muhimu zinapatikana
isipokuwa dawa za maumivu na Anti biotic zinatumika kwa wingi hivyo
baadhi ya wakati zinakwisha bila ya kuingizwa nyengine.
Ameahidi
kuwa dawa hizo zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya wananchi
na atahakikisha kuwa hakutatokea ubadhirifu wowote ulio nje ya
utaratibu uliopangwa na Wizara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment