Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016
amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es
Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana
tarehe 02 Oktoba, 2016.
Kabla ya Uteuzi
huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
03 Oktoba,
2016
0 comments:
Post a Comment