Botswana ni nchi ya kwanza kutoka Afrika imetangaza hadharani
kutoridhishwa na uamuzi wa Afrika Kusini kuondoka ICC na kuthibitisha
kuwa itaendelea kushirikiana na kutoa msaada kwa mahakama hiyo ya
kimataifa .Wizara ya mambo ya nje ilichapisha habari hiyo mitandaoni na kusema kuwa imehuzunishwa na uamuzi wa Afrika Kusini .
Mataifa
mengi ya Afrika kama frika Kusini,Burundi ,Gambia na kadhalika ambayo
ni wanachama wa mahakama ya Hague kwa muda wa mwezi mmoja wamekuwa
wakitangaza kujiondoa kutoka kwa uanachama wao na ICC .
Uamuzi huo umesababishwa na madai kuwa ICC imekuwa ikifanya ubaguzi hasa dhidi ya viongozi wa Afrika .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment