Mkataba
huo umefanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na mashirika ya kimataifa,
mabalozi wa nchi za umoja wa ulaya, viongozi wa serikali ya Tanzania na
Uganda ambapo katika mchakato huo waziri wa nishati na madini wa
Tanzania Profesa Sosypeter Muhongo na waziri mwenzake wa Uganda Irine
Muloni wamewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utaimarika na kukamilika
mwaka 2020.
Naye
waziri wa mafuta wa jamhuri ya kidemkrasia ya Congo Profesa Aime Mukena
amewataka wafanyabishara wa Tanzania hasa wanaojihusisha na mafuta
kwenda kuwekeza katika nchi yao kufuatia changamoto ya uhaba wa bohari
za mafuta zinazoikabili baadhi ya mikoa katika taifa la Congo.
Kufuatia
hatua hiyo baadhi ya wawekezaji wa nishati na madini nchini
wameihakikishia serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuwa
wameanza kusaidia nchini kuongeza hifadhi za mafuta huku wakiendelea na
bomba la mafuta kutoka Uganda kuja jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment