Meneja
wa Miradi wa Shirika la Plan International - Geita, Gratian Kweyamba
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya malengo ya Mradi
wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto, kulia ni
Mratibu wa Mradi huo, Maxmillian Kitigwa. Mradi huu wa miaka mitatu
unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na
Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa
Geita............................................................................................................................
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Geita
Shirika
la Plan International limetoa rai kwa Serikali kuanzisha Idara ya Kazi
katika maeneo ya migodi ili ishirikiane na wachimbaji wa madini
kuhakikisha tatizo la ajira kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18
linakoma.
Hayo yamesemwa leo mkoani Geita na Mratibu wa Mradi wa
Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto wa shirika
hilo, Maxmillian Kitigwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu
ya changamoto zinazoukabili mradi huo.
Kitigwa amesema kuwa katika
Mkoa huo kuna changamoto nyingi zinazowakabili watoto lakini kukosekana
kwa Idara ya Kazi katika maeneo ya migodi kunasababisha uvunjwaji mkubwa
wa haki za watoto kwa kuwa watoto wengi wanakimbilia kufanya shughuli
mbalimbali katika maeneo hayo ili kujipatia kipato.
”Sasa hivi Geita
imeshakuwa Mkoa, na mkoa huu umezungukwa na migodi mikubwa hivyo
Serikali inatakiwa kuweka Idara ya Kazi katika sehemu hizi ili kuzuia
ajira za watoto pamoja na kukomesha unyanyaswaji unaofanywa kwa baadhi
ya watu wanaofanya kazi huko”, alisema Kitigwa.
Mratibu huyo
amewaomba wananchi wa Mkoa huo waache kutatua matatizo kiundugu na
badala yake watoe ushirikiano kwa kuripoti matukio mabaya yanayofanyika
katika maeneo yao na kuyafikisha katika ngazi ya mkoa ili yafanyiwe
kazi.
Naye Meneja wa Miradi wa Shirika hilo kwa Mkoa wa Geita,
Gratian Kweyamba amesema kuwa mradi huo unalengo la kuhakikisha watoto
wanalindwa na kuondolewa katika mazingira hatarishi hivyo, Serikali
isaidie katika kutatua changamoto hii na kuwarudisha watoto katika
makuzi mazuri.
“Ingawa rasilimali tulizonazo ni chache kuliko
mahitaji ya watoto lakini tunajitahidi kuwajengea uwezo Serikali na
wadau mbalimbali ili waweze kushiriki katika kuimarisha mfumo mzima wa
ulinzi wa watoto na kuwafanya wakuwe katika mazingira bora”, alisema
Kweyamba.
Mradi huu wa miaka mitatu unafadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kuratibiwa na Shirika la Plan
International, unatekelezwa Mkoani Geita katika Wilaya za Chato, Geita
na Nyan’ghwale ukiwa na lengo la kuondoa ajira hatarishi na vitendo vya
ukatili kwa watoto wanaoishi karibu na maeneo ya migodi, umeanzishwa
Novemba 2015 na utagaharimu jumla ya Euro 1,500,000 hadi kuisha kwake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment