RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, ametoa miezi miwili kwa taasisi zote zinazohusika na ujenzi wa
ofisi ya Zimamoto zinazojengwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume, Zanzibar, ziwe zimekamilisha ujenzi huo.
Agizo hilo alilitoa jana baada ya kutembelea eneo lililotengwa kwa
ajili ya ujenzi wa ofisi ya Zimamoto katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume, ujenzi ambao unaonekana kusuasua kwa
muda mrefu.
Dk. Shein alizitaka taasisi husika kukamilisha ujenzi huo ndani ya
kipindi hicho hasa ikizingatiwa wahusika walipewa agizo hilo Mei mwaka
jana wakati alipotembelea uwanja huo.
Alisema tangu kipindi hicho hadi leo ujenzi huo haujaanza na
kusisitiza ni lazima ukakamilike katika kipindi hicho hasa ikizingatiwa
serikali imekwisha kutoa Dola za Marekani milioni 3.5 kwa ajili ya
ununuzi wa gari za zimamoto na dola milioni 1.5 ambazo zimetolewa na
Benki ya Dunia kwa ajili ya nununuzi wa gari hizo.
“Tusifanye kazi kwa utamaduni tuliozoea, nimekupeni muda mrefu miezi
miwili, malizeni mkimaliza nitakuja, hamkunialika nitakuja mkinialika
nitakuja…fedha zipo lakini hamjaziomba,” alisema Dk. Shein.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na
Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir alimueleza Dk. Shein haja ya
kuwapo ushirikiano kwa taasisi zote zinazosimamia ujenzi huo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment