SERIKALI ya Japan imetoa Sh bilioni 170 kwa ajili ya uboreshaji wa
miundombinu na kuweka vifaa vya huduma bora katika Kituo cha afya
Murangi katika Jimbo la Musoma vijijini.
Fedha hizo zilitolewa jana na Balozi wa Japan nchini, Masaharu
Yoshida ambaye alisema lengo ni kuiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma
stahiki kwa kila mwananchi.
Alisema fedha hizo zitatumika kuboresha miundombinu, kujenga nyumba
za wauguzi, choo cha wagonjwa, shimo la kutupia kondo la nyuma na
kurekebisha tanuru la kuchomea takataka za hospitali ikiwa lengo ni
kuweka mazingira safi na salama kwenye kituo hicho.
Yoshida alisema suala la afya ni jambo la msingi kwa maisha ya binadamu.
Alisema msaada huo unatokana na ombi la Mbunge wa Musoma
Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na
Madini.
Yoshida alisema ikiwa kituo hicho kitafanyiwa marekebisho kitasaidia
kuondoa usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu
kutafuta huduma huku wauguzi wakiishi mbali na sehemu yanakofanyia
kazi.
“Ninafuraha kubwa na ni heshima kwangu kusaini mkataba wa mradi huu
mpya kupitia mfuko wa mpango wa miradi midogo kwa ajili ya usalama wa
binadamu, hivyo basi tunatoa Sh bilioni 170 kwa ajili ya uboreshaji na
ununuzi wa vifaa tiba.
“Tumepata taarifa wananchi wengi wanahudumiwa kwenye kituo hiki na
wengine wanatoka mbali zaidi, naamini baada ya mradi huu kukamilika
hudumu muhimu zitapatikana hapa na zitakuwa zinawasaidia wananchi
wengi,” alisema Yoshida.
Alisema Japan itaendelea kutoa michango yake katika kusaidia kituo hicho cha afya kusaidia upatikanaji wa huduma mbambali.
Naye Profesa Muhongo alisema mradi huo utachukua mwaka mmoja
kukamilika na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na imani naye ikiwa ni
pamoja na kushirikiana ili aweze kutimiza ahadi zake.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Anarose Nyamubi ambaye alimwakilisha Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Dk.Charles Mlingwa, alisema uboreshwaji wa kituo hicho
utakuwa ni suluhisho katika kuboresha afya ya wananchi.
Alisema viongozi wengine wanapaswa kuiga mfano wa Profesa Muhongo kwa
kufanya juhudi za kukutana na wadau mbalimbali katika kutaka kuwasaidia
wananchi wanao waongoza.
Home
News
Slider
Japan yatoa Sh. bilioni 170 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu Musoma vijijini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment