Mwanafunzi wa Kiislamu afukuzwa shuleni na kuzuiwa kufanya mtihani kwa kukataa kuvua hijabu nchini CanadaMwanafunzi
mmoja wa Kiislamu ameripotiwa kufukuzwa shuleni na kuzuiwa kufanya
mtihani na mwalimu mmoja baada ya kukataa kuvua hijabu shuleni nchini
Canada.
Tukio hilo lilizuwa utata baada ya kutokea kwenye shule ya upili ya College de Maisonneuve iliyoko mjini Montreal.
Msemaji wa shule hiyo Line Legare alitoa maelezo na kusema, ‘‘Mwalimu wetu wa somo la biyolojia aliwahi kutangaza mwanzoni mwa mwaka kwamba hatoruhusu wanafunzi wake kuingia kwenye mtihani wakiwa na kofia, mtandio au hijabu vichwani. Mwalimu huyo alimfukuza mwanafunzi kutokana na ukiukaji wa sheria iliyowekwa kwa hofu ya uwezekano wa kulaghai kwenye mtihani.’’
Maelezo zaidi yamearifu kwamba mwanafunzi huyo alifukuzwa baada ya kukataa kuvua hijabu kutokana na sheria za imani ya dini yake ya Kiislamu.
Legare aliongezea kuwa tukio hilo limemkera mwalimu na hivyo basi, wanaendelea kujadili ili mwanafunzi huyo aweze kufanya mtihani katika tarehe nyingine.
Legare pia alisema kwamba mwanafunzi huyo bado hajawasilisha rasmi mashtaka dhidi ya mwalimu na kwa sasa utawala wa shule unafanya mazungumzo ili kuhakikisha tukio kama hilo halirudiwi tena.
Kwa upande mwingine waziri mkuu wa mkoa wa Quebec Philippe Couillard naye alitoa maelezo na kubainisha kuridhishwa kwa utatuzi wa mzozo huo huku akiahidi kuwasilisha muswada bungeni kuhusu tukio hilo.

0 comments:
Post a Comment