KAMATI ya Katiba na Sheria imekataa mapendekezo ya ongezeko la faini kwenye Sheria ya Makosa ya Barabarani ya mwaka 1973 kutoka Sh.10,000 na Sh.50,000 hadi kufikia Sh.200,000 na Sh.500,000 kwa maelezo kwamba ongezeko hilo halitapunguza ajali.
Hayo yalijitokeza jana wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokuwa kikijadili Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2016.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchegerwa, alisema taarifa ya mapendekezo ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra) ya kubadilisha sheria hiyo, haina mashiko kwani ina mapungufu makubwa na ipo kimaslahi zaidi.
Kutokana na hali hiyo, alisema kamati haiwezi kukubaliana na maombi ya Sumatra kwa kuomba kubadilisha sheria na badala yake wanatakiwa kupitia maombi yao upya ili waone jinsi gani ya kuondokana na ajali kwa kutoa elimu kwa madereva na si kuongeza faini.
0 comments:
Post a Comment