Image
Image

Kasika: Posho za Mwenge sasa kujenga shule


MKUU wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Majura Kasika, ameagiza posho iliyookolewa kutokana na zuio la ushiriki wa maofisa wa wilaya hiyo kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Simiyu Oktoba 14, mwaka huu, zielekezwe katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo vya shule.
Majura amesema kutokana na zuio hilo la Rais John Magufuli lililogusa wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na masaidizi wao, Sh. milioni 2.08 zimeokolewa.
Amesema kiasi hicho cha fedha kitasaidia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo vya Shule ya Msingi Lumbanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment