Kiongozi
mkuu wa chama cha upinzani cha Renamo nchini Msumbiji amesema mmoja wa
viongozi wa juu wa chama chake amepigwa risasi na kufa katika ufukwe wa
mjini Maputo.
Jeremias Pondeca ndiye anayerdaiwa kuuawa na alikuw
mjumbe wa kamati maalumu ya kujaribu kuondoa tofauti kati ya serikali na
chama hicho.
Haijafahamika mara moja kuwa ni nani aliyemuua kiongozi huyo aliyekuwa akifanya mazoezi katika eneo hilo la ufukwe.
Kumekuwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na Renamo tangu kuzuka kwa mvutano kufuatia miaka miwili iliyopita.
Pande hizi mbili zilizusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 16 yaliyomalizika mwaka 1992.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment