Vikosi
vya usalama nchini Myanmar vimesema kuwa watu 17 wameuawa wakiwemo
polisi tisa, mauaji hayo yametokea katika kituo cha polisi huko katika
mpaka wa nchi hiyo na Bagladesh
Afisa mmoja wa Polisi amewaambia
waandishi wa habari kuwa miongoni mwao ni washambuliaji wanane ambao
waliuawa wakati wa mapambano katika jimbo la Rakhine.
Imeelezwa kuwa washambuliaji wawili walikamatwa.
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na jamii ndogo ya kiislamu ya Rohingya.
Kumekuwa na mvutano mkali katika Jimbo la Rakhine kati ya jamii ya Budha na jamii ya kiislamu ya Rohingya.
Shambulio la hivi karibuni linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea jimboni Rakhine tangu mwaka 2012.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment