Dar es Salaam. Shirika
lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya elimu nchini, Haki
Elimu limelaani kitendo cha adhabu ya kikatili iliyotolewa na walimu wa
mafunzo kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Mbeya Day,
Sebastian Chinguku.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John
Kalage alisema vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi
hususani wa kike kuacha shule hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kupata
elimu.
Alisema serikali ihakikishe kuwa miongozo yake ya kusimamia na kuimarisha nidhamu shuleni inazingatiwa na watu wote.
"Serikali
inapaswa kuanzisha mifumo rasmi ya kutoa taarifa dhidi ya matukio ya
ukatili yanayoendelea katika shule zetu itakayowawezesha wanafunzi na
wadau wengine kutoa taarifa mara wanapokutana na matukio ya kikatili
kama haya kwa lengo la kuyakomesha," alisema Kalage.
0 comments:
Post a Comment