WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amemtaka Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
(DCI), Diwani Athumani, wajihusishe kikamilifu kwenye upelelezi wa kesi
ya mauaji ya wataalamu wa utafiti yaliyotokea mkoani Dodoma.
Dk Mwakyembe alisema hayo Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu mauaji ya wataalamu hao, yaliyotokea
katika kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino.
Wataalamu wawili wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian Arusha (Sari) na dereva, waliuawa kikatili Oktoba Mosi, mwaka huu.
Alisema Jamhuri itahakikisha inadai adhabu kali kwa kila mtuhumiwa
ili kutoa fundisho kwa wananchi wote, kwa kuwa tabia ya kujichukulia
sheria mkononi hailipi.
Watafiti waliouawa ni Teddy Lumanga, Jaffari Mafuru na dereva wao Nicas Magazine.
“Pia wizara inaviomba vyombo vyote vya habari kuisaidia serikali
katika kampeni hii dhidi ya utaratibu huu batili wa kujichukulia sheria
mkononi hasa ikizingatiwa kuwa waandishi wa habari wenyewe wamo kwenye
kundi la wanataaluma mbalimbali wanaokwenda kila sehemu nchini
wakilindwa na utawala wa sheria.
Alisisitiza kuwa ili kukomesha wimbi hili la wananchi kujichukulia
sheria mkononi, wizara yake itachukua kila hatua inayowezekana
kuhakikisha kuwa wote waliohusika kushawishi, kuhamasisha au kuchochea,
kupanga, kushambulia kwa mapanga na kushiriki kuchoma moto katika tukio
hilo, wanafikishwa mahakamani kuvuna walichopanda.
Awali alisema wizara yake imesikitishwa na kushtushwa na ongezeko la
matukio ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, kwa visingizio
mbalimbali kwa kuwa huo ni ukiukwaji wa utawala wa sheria ambao msingi
serikali ina wajibu wa kuulinda.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment