LINAPOKUJA suala la maradhi ya moyo, wengi wetu watakuwa wamesikia
visababishi vyake, na hivyo kujitahidi kuviepuka ili kukaa mbali na
uwezekano wa kuyapata.
Miongoni mwa visababishi vya maradhi hayo ni pamoja na staili mbovu
ya ulaji wa aina fulani ya vyakula, ambavyo ingawa hatukatazwi kuvila
bali kuviingiza tumboni kwa wingi.
Vyakula hivyo ni pamoja na nyama na bidhaa zinazotokana na maziwa zenye wingi wa mafuta.
Hata hivyo, utafiti mpya uliochunguza tabia za mlo na maradhi ya moyo
katika mataifa 42 ya Ulaya kwa kipindi cha miaka 16, unapingana na
dhana hiyo tuijuayo kwa miaka mingi sasa.
Kwa maana hiyo unapingana na miongozo ya afya iliyowekwa na serikali
za mataifa mengi linapokuja suala la kukabiliana na maradhi ya moyo.
Utafiti huo pamoja na mambo mengine umeonya ulaji wa viazi mviringo
au vyakula vinavyotokana na viazi kama vile chipsi kwa wingi huongeza
hatari ya kusababisha maradhi ya moyo.
Ulisema pia mazao ya nafaka yanaongeza hatari hiyo, huku ukionesha
mazao kutokana na maziwa husaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi
hayo.
Lakini pia unapinga dhana kuwa ulaji wa nyama kwa wingi husababisha maradhi hayo.
Dk. Pavel Grasgruber, mwandishi kiongozi wa ripoti ya utafiti huo
kutoka Chuo Kikuu cha Masaryk nchini Jamhuri ya Czech, alitoa mwito wa
ushauri na mwongozo mpya kutolewa kuendana na utafiti huo.
“Hatari ya kupata maradhi ya moyo tuijuayo sasa imetokana na takwimu
zisizo sahihi. Utafiti huu mpya ulikuwa wa kina na una hekima ya
matumizi ya mlo sahihi.”
“Ni wazi kabisa matumizi ya mazao ya maziwa na nyama hayahusiani na hatari ya maradhi ya moyo, kama inavyoaminika kwa wengi.
“Tatizo kubwa ni wingi wa matumizi ya vyakula vya nafaka, mtama na viazi.
“Nina wajibu wa kutoa mapendekezo kwa watu kubadili milo yao na kupunguza ukubwa wa wanga wao mwilini.”
Utafiti huo ambao ulilinganisha takwimu kutoka nchi tofauti,
ulionesha mahali ambako kuna matumizi makubwa ya vyakula vya wanga,
kulikuwa na kiwango kikubwa cha maradhi ya moyo.
Pia ulionesha kuwa nchi zenye kiwango cha chini cha maradhi ya moyo
zilikuwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya mlo wenye utajiri wa mafuta
na protini.
Takwimu zilizochapishwa katika Jarida la Utafiti wa Vyakula na
Virutubisho zimeonesha mazao kutokana na maziwa yenye kiwango kikubwa
cha mafuta hasa jibini vilifanya kazi ya kupunguza marathi ya moyo.
Matunda jamii ya machungwa, mvinyo, jamii ya karanga, olive na mbogamboga, zote pia zimeonekana kuwa na uwezo wa kulinda moyo.
Utafiti ulionesha kwamba mwenendo wenye kuhatarisha zaidi maradhi ya moyo ni mlo wenye wanga, viazi mviringo na nafaka.
Dk. Grasgruber alisema kuwa utafiti unapingana na utamaduni na
ufahamu wetu wa miaka mingi kuhusu vyakula vyenye mafuta yenye
kusababisha madhara mwilini (saturated fat).
Kama utakumbuka mafuta haya ambayo kwa kawaida huganda katika mazingira ya kawaida ya joto la ndani hutokana na wanyama.
Ni tofauti na yale ‘unsaturated fat’, ambayo hupunguza lehemu mwilini
na hivyo kupunguza uwezekano wa kupatwa na maradhi ya moyo, kiharusi,
uzito mkubwa, kisukari na shinikizo la damu.
Unsaturated fat hupatikana zaidi kutokana na mazao ya mimea.
Mwongozo kuhus mlo salama wa Uingereza ulioanzishwa mwaka 1983, kwa
mfano unashauri ulaji zaidi wa vyakula vya wanga ikiwamo viazi mviringo
na nafaka.
Na unatoa ushauri watu ulaji kidogo wa vyakula vyenye mafuta hasa saturated fat.
Utafiti mwingine uliochapishwa Mei mwaka huu pia unatambua viazi kama chanzo cha hypertension, yaani shinikizo la juu la damu.
Utafiti huo ulibainisha kwamba ulaji wa viazi mara nne kwa wiki
unaweza kuwa hatarishi na kuchangia hali inayosababisha kiharusi na
maradhi ya moyo, ambayo ni wauaji wakubwa nchini Uingereza.
Utafiti huo unaendana na mwingine uliowahi kutoa matokeo ya
kustaajabisha ukionesha mataifa ambayo hutumia mvinyo na nyama kwa
wingi watu wake huishi maisha marefu zaidi kulinganisha na yale
yanayotumia zaidi wanga.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment