MAPERA ni matunda yanayopatikana kwa wingi licha ya kutopendwa na
watu wengi kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na
mbegu mbegu nyingi.
Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C
pamoja na vitamin A na inaelezwa kuwa kiwango cha vitamin C
kinachopatikana ndani ya mapera ni sawa na mara nne ya kiwango cha
vitamin hiyo inayopatikana kwenye machungwa na maembe.
Kama yalivyo matunda mengine kuwa na faida mbalimbali katika mwili wa
binadamu, mapera nayo ni miongoni mwa matunda hayo kutokana na kuwa
faida nyingi ikiwamo kusaidia kurutubisha mayai ya uzazi kwa kuwa yana
madini yaitwayo Folate.
Pia yana uwezo wa kuzuia ugonjwa wa kisukari kutokana na wingi wa
fibre ambayo husaidia kupunguza kiasi cha sukari katika damu, vile vile
husaidia kusafisha mfumo kwa usahihi.
Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa na Jarida la Journal of
Human Hypertension mwaka 1993, mapera yanaweza kupunguza kiwango cha
msukumo mkubwa wa damu ndani ya mwili, hii ni kwa sababu matunda hayo
kuwa na madini ya potassium na vitamin C ambayo husaidia kuweka sawa
msukumo wa damu ndani ya mwili.
Pia majani ya mpera yanapoandaliwa kama chai yaani yakichemshwa
husaidia kuondoa sumu mwilini, jambo ambalo husaidia kulinda afya ya
moyo wako.
Pia husaidia wale wenye tatizo la kuharisha hii ni kwa mujibu wa
utafiti wa mwaka 2008 uliochapishwa kwenye Jarida the Revista do
Instituto de Medicina Tropical de São Paulo, ambao walieleza kwamba
majani hayo ya mapera yanauwezo wa kuzuia vimelea vya staphylococcus
aureus ambavyo huchangia tatizo la kuhara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment