WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mji wa Dodoma ni lazima upangwe ili uwe tofauti na miji mingine hapa nchini.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati
akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah
ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kuelezea
nia yake ya kutaka kuwekeza mjini Dodoma.
Amesema Serikali haitaki
kurudia makosa yaliyofanyika kwenye miji mingine. “Katika kuupanga ule
mji, ni lazima mji upangwe kama ambavyo miji mingine mikuu inapangwa.
Kila eneo kutakuwa na nyumba za aina fulani. Hatuwezi kuachia watu
wajenge popote na wanavyotaka, mji unakuwa haupangiki. Na hilo ndilo
kosa lililofanyika kwenye miji mingine mikubwa ambayo tunayo kwa sasa.”
Amesema
Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya kuhamia Dodoma imepewa jukumu la
kupitia upya Master Plan ya mji wa Dodoma na kuainisha maeneo ambako
nyumba za aina mbalimbali zitajengwa.
“Kimsingi tunataka tuanze
kujenga miji iliyopangiliwa na Dodoma tunataka uwe wa mji kwanza
kuujenga vizuri kwa standard ya sasa. Kutakuwa na nyumba za ghorofa
katika maeneo fulani, na nyumba za kawaida katika maeneo fulani.
Mkurugenzi wa CDA amekwishaandaa ramani rasmi,” amesema.
Akizungumzia
kuhusu ujenzi kwenye maeneo ambayo tayari wananchi wanaishi, Waziri
Mkuu amesema Serikali itaweka utaratibu ili kuwe na mikataba baina ya
mwekezaji na mwananchi anayemiliki eneo husika ili asinyimwe haki ya
kumiliki eneo lake.
“Kama tutahitaji eneo ambalo tayari lina makazi,
taratibu zetu ni zilezile kwamba tutaweka mikataba kati ya mwekezaji na
mwananchi. Kama anataka kujenga kwenye eneo lile, basi lazima amhusishe
mwenye eneo na kama anataka kujenga ghorofa ni lazima ahakikishe mwenye
eneo anapata umiliki kama tulivyofanya kule Magomeni,” amesisitiza.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba
wako tayari kushirikiana na Serikali katika zoezi la Serikali kuhamia
Dodoma kwa lengo wa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata
makazi bora na ya kudumu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment