Image
Image

Mkutano wa kwanza wa kamati ya uchunguzi ya TBMM dhidi ya jaribio la mapinduzi wafanyika

Bunge la kitaifa nchini Uturuki TBMM limemteuwa mbunge wa chama tawala cha AKP Reşat Petek kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi dhidi ya jairbio la mapinduzi ya FETO/PDY ya Julai 15.Kamati hiyo ya uchunguzi iliyoundwa bungeni baada ya jaribio la mapinduzi ya Julai 15 ilifanya mkutano wake wa kwanza.
Katika mkutano huo, mwenyekiti aliweza kuwateuwa wawakilishi wa nafasi ya naibu msaidizi wake, msemaji na katibu wa kamati.
Selçuk Özdağ alichaguliwa kuwa naibu msaidizi huku Mihrimah Belma Satır akichaguliwa kuwa msemaji wa kamati.
Serkan Bayram naye alichaguliwa kuchukuwa nafasi ya katibu wa kamati.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment