Image
Image

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki yakashifu uamuzi wa Iraq wa kurefusha muda wa kuhudumu kwa jeshi.

Bunge la serikali ya Iraq limetangaza kupinga pendekezo la bunge la Uturuki kuhusu suala la kurefusha muda wa kuhudumu kwa jeshi lake nchini humo.Kufuatia uamuzi wa bunge la Iraq lililokataa kuidhinisha, Uturuki ilikashifu hatua ya Iraq na kukemea vikali bunge lao.
Wizara ya mambo ya nje ilitoa maelezo na kuafahamisha kwamba serikali ya Uturuki imekuwa ikiunga mkono Iraq kwa kila jambo na kusaidia wananchi wake kwa miaka mingi.
Maelezo zaidi yaliarifu kwamba Uturuki itaendeleza harakati zake kwa lengo la kupambana dhidi ya makundi ya kigaidi hasa DAESH ambalo limekuwa ni tishio la usalama kimataifa.
Maelezo hayo pia yalisema, ‘‘Uturuki imekuwa na nia ya kutaka kusaidia nchi jirani ya Iraq ambayo maelfu ya wananchi wake wamekuwa wakikumbwa na matatizo kutokana na vitisho vya kigaidi. Kwa miaka mingi Uturuki imekuwa ikijitahidi ili kuhakikisha ardhi ya Iraq inapata ulinzi kamili, amani na utlivu.’’
Wawakilishi wa bunge la Iraq nao walitoa maelezo na kusema kwamba nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia makubaliano mapya na kanuni mpya zilizowahi kuafikiwa mwaka 2007 kwa mara ya kwanza na bunge la TBMM nchini Uturuki.
Hapo jana, bunge la Iraq lilituma ujumbe kwa ubalozi wa Uturuki mjini Baghdad na kuarifu kupinga uamuzi wa TBMM wa kutaka kurefusha muda wa kuhudumu kwa jeshi nchini humo kwa lengo la kutoa mafunzo ya kijeshi dhidi ya DAESH.
Hatua hiyo ya kupinga uamuzi wa Uturuki pamoja na kukashifu maelezo ya rais Recep Tayyip Erdogan inaweza kuathiri uhusiano wa kibiashara na uchumi kati ya Uturuki na Iraq.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment