Image
Image

Muungano wa Kiarabu walaani vikali mashambulizi ya utawala wa Syria dhidi ya raia.

Muungano wa Kiarabu umekemea na kulaani vikali mashambulizi ya utawala wa Syria yanayotekelezwa dhidi ya raia mjini Aleppo.Muungano huo ulifanya mkutano wa dharura katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri ili kujadili hali hiyo ya mauaji kufuatia wito wa serikali ya Kuwait.
Viongozi wote na wawakilishi wa mataifa ya Kiarabu waliohudhuria mkutano wa dharura walijadili mapigano yanayoendelea Syria na kusisitiza kwamba mzozo huo unaweza kutatuliwa kwa njia ya kisiasa pekee.
Viongozi pia walibainisha kuendelezwa kwa mashambulizi dhidi ya raia Aleppo na katika miji mengine ya Syria inayopelekea wakaazi kuwa katika hali mbaya zaidi.
Viongozi pia walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukuwa hatua ya haraka ya kuanzisha mchakato wa kusitisha mapigano, na kuhimiza mashirika ya umma kutoa misaada ya kibinadamu.
Katika mkutano huo, makundi ya kigaidi kama vile DAESH na Nusra yalilaaniwa na kukemewa vikali kwa kuchangia mauaji ya raia na kukiuka haki za kibinadamu.
Muungano wa Kiarabu ulitoa wito wa kufikishwa kwa magaidi mbele ya vyombo vya sheria na kufunguliwa mashtaka kwa madai ya kutekeleza mauaji na kuchochea vita.
Muungano huo pia ulitoa wito kwa baraza la usalama la UN kuingilia kati mchakato wa mazungumzo ya amani Syria na kuhakikisha mkataba wa kusitisha mapigano umezingatiwa.
Wakati huo huo, muungano huo pia uliarifu hali hiyo iliyopo Syria kuwa ni tishio kubwa la usalama wa kanda, na kutoa ombi la kufanya mkutano na baraza la UN ili kutafuta suluhisho la haraka kuhusu matukio yanayojiri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment