WATU wanaokaa kitako zaidi ya saa nne wamo katika hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.
Utafiti unaonyesha watu wanaokaa sehemu moja kwa zaidi ya saa nne
wanakabiliwa na magonjwa ya kisukari, moyo, shinikizo la damu na
saratani.
Dk. Fredirick Mashili wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
(MUHAS) alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumzia kampeni ya
mazoezi na afya bora itakayofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
“Ingawa teknolojia ya kisasa imerahisisha maisha lakini kadri muda
unavyokwenda imefanya watu wengi kuishi maisha ya kukaa tu bila kufanya
mazoezi ya kutosha na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata magonjwa
hayo,” alisema.
Akitoa mfano, alisema katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni
yenye kichwa cha habari ‘International Cardiovascular Desease
Statistics’ Shirika la Moyo la Marekani limeeleza kuwa kutokufanya
mazoezi na kula vyakula visivyofaa ni mambo yanayochangia magonjwa ya
moyo.
Alisema mabadiliko ya uchumi, watu kuhamia mijini, ustawi wa viwanda
na kuenea kwa biashara za kimataifa huleta mabadiliko katika mtindo wa
maisha hasa mijini kwa kusababisha kuongezeka magonjwa yasiyo ya
kuambukiza.
“Watu wanakaa ofisini muda mrefu mbele ya kompyuta zao, wakitoka
wanaingia kwenye gari kwenda nyumbani, wakifika wanakaa kutazama
luninga, matokeo yake wanajikuta wamepata maumivu ya mgongo… hali ni
mbaya,” alisema.
Alisema kukua kwa teknolojia kumechangia pia watoto kukosa muda wa
kucheza badala yake hupendelea kukaa na kucheza michezo ya kwenye
kompyuta na video (luninga).
Alisema watoto wasiofanya mazoezi wanaweza kukabiliwa na hatari ya kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na mfadhaiko mkubwa.
“Upo uwezekano mkubwa wa watoto hawa kuwa wavutaji wa sigara na
kutumia dawa za kulevya wanapokuwa wakubwa kuliko watoto wanaofanya
mazoezi.
“Na watu wazima wasiofanya mazoezi wanapofikia umri wa uzee hupoteza
nguvu na uwezo wa kufanya shughuli za kila siku na akili zao huzorota,”
alisema.
Home
Afya
Slider
Utafiti unaonesha watu wanaokaa sehemu moja kwa zaidi ya saa nne wanakabiliwa na magonjwa ya kisukari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment