Baada
ya mashabiki wa Simba kuvunja viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa
Simba na Yanga uliopigwa Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli ya
moja kwa moja, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, Nape Nnauye
Imepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika na timu za Yanga na Simba.
Waziri
Nape amefanya maamuzi hayo baada ya jana Jumapili kufanya ziara katika
uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea juzi Jumamosi .
Amesema
kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu
hizo haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali
itawaruhusu.
“Uwanja huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka pale
tutakapoamua vinginevyo hapo baadae, hawatatumia uwanja huu watafute
viwanja vingine, sababu hapa kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za
watanzania.
“Wanaotakiwa kutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo
ni wengi kuliko Yanga na Simba, wapo wengine ambao ni wastaarabu
wanaweza kutumia uwanja huu,” aLIsema Waziri Nape.
Maamuzi mengine ni
Simba kutakiwa kulipia gharama ya viti 1,781 vilivyoharibika, Simba
haitapata mgao wa mchezo hadi walipe gharama za uharibifu, kamera za
CCTV zitafungwa uwanja mzima na Yanga itatakiwa kulipa gharama ya mageti
manne ya upande wa mashabiki wake yaliyovunjwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment