RAIS Dk. John Magufuli, amemteua aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumwakilisha katika mkutano
wa makazi wa Habitat III unaofanyika katika mji wa Quito, Ecuador.
Taarifa aliyoituma kwenye mitandao ya jamii na Profesa Tibaijuka
jana, ilisema katika msafara huo amefuatana na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, Dk. Yamungu Kayandabila.
“Hivi sasa niko Geneva, Uswisi kwa matayarisho nikielekea Quito
Ecuador mkutano wa makazi duniani wa HABITAT III kumwakilisha Rais wetu
nikiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,namshukuru Rais kwa
heshima hii kubwa, Sitamuangusha.
Habitat III,ni mkutano wa uamuzi na mustakabali wa Shirika la Makazi Duniani na agenda ya maendeleo endelevu ya miji.
“Kama tunavyojua mkutano wa Habita I ulifanyika Vancouver,Canada
mwaka 1976, Habitat II ulifanyika Istanbul, Uturuki mwaka 1996 na huu
Ecuador Marekani ya Kusini 2016,”alisema.
Alisema kila baada ya miaka 20 wakuu wa nchi hukutana kukubaliana
namna ya kuendeleza makazi kupitia Shirika la UNHABITAT ambalo aliwahi
kuliongoza kwa miaka 10.
“Rais Magufuli alichaguliwa na kuongoza Baraza la Uongozi wa shirika
hilo (Governing Council) kwa muhula wa mwaka 2006/2008 alipokuwa Waziri
wa Ardhi.
“Wafanyakazi walimpenda kiasi kwamba alipobadilishwa wizara na
kupelekwa Mifugo na Uvuvi karibu iwe zogo ofisini kwangu wakidai
tutayumba.
“Niliwatuliza na kuwaambia kumbadilisha wizara hakumuondolei
uenyekiti wake na kweli aliendelea nao na kumaliza,”alisema Tibaijuka.
Alisema katika mkutano huo, jambo kubwa akalolipigania ni utaratibu
wa shirika hilo kuzisaidia nchi zinazoendelea kama sisi kwa kuzikopesha
halmashauri zao fedha za miundombinu, bila kuilazimisha Serikali kuu
kutoa dhamana kwa mikopo hiyo.
Alisema jambo hilo ni la msingi kwa vile huleta kasi ya maendeleo
ingawa huwa linapingwa na wakubwa wanaotaka kukopa kupitia Serikali kuu
ili waibane kwa kutumia Benki ya Dunia, kitendo ambacho
kinachelewesha kasi ya maendeleo.
“Tutajitahidi kulingana na maelekezo ya Rais tunayemwakilisha kuhusu
msimamo wa nchi yetu na washirika wake ambao ni nchi za Afrika na za G77
na China,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment