KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, wakati wowote
inatarajia kutoa uamuzi kuhusu sakata la usajili wa beki, Hassan
Ramadhani ‘Kessy’, baada ya kupokea ripoti ya klabu za Simba na Yanga.
Kessy alisajiliwa na Yanga kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania
Bara msimu huu, lakini Simba iliwasilisha pingamizi ikidai kuwa
wapinzani wao wamemsajili beki huyo bila kufuata taratibu.
Klabu ya Simba inadai kuwa Kessy alivunja mkataba kwa kuanza kufanya
mazoezi na mahasimu wao Yanga pamoja na kusaini mkataba wa kuichezea
timu hiyo kabla ya ule aliosaini akiwa kwa Wekundu wa Msimbazi
kumalizika Juni 15, 2016.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema kamati hiyo itakutana ndani ya
siku mbili zijazo ili kutoa ufafanuzi wa ripoti hiyo kulingana na
kanuni.
“Kamati ilizitaka klabu za Simba na Yanga kukutana ndani ya siku tatu
ili kujadili suala la Kessy ili ziweze kufikiana makubalino na kutoa
ripoti ambayo tayari wameiwasilisha,” alisema.
Lucas alisema kamati hiyo itachelewa kukutana kuipitia ripoti hiyo na
kutoa uamuzi kwa kuwa viongozi na wajumbe wameajiriwa kwenye sekta
nyingine tofauti na TFF, hivyo kubanwa na majukumu ya kikazi.
Awali kamati hiyo ilitarajia kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Septemba 4 mwaka huu, lakini ikashindikana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment