Image
Image

Rais Erdoğan na Obama wafanya mazungumzo ya simu na kujadili suala la mapambano dhidi ya ugaidi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amefanya mazungumzo ya simu na rais mwenzie wa Marekani Barack Obama.Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili suala la mapambano yanayoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la DAESH.
Kulingana na vyanzo vya ofisi ya rais, rais Obama aliipongeza Uturuki na kutoa shukrani kubwa kwa ushirikiano wao kwenye harakati za mapambano dhidi ya DAESH na kuunga mkono vikosi vya upinzani wa utawala wa Syria.
Rais Obama pia aliarifu kuridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya Uturuki na Iraq katika operesheni na mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo.
Rais Erdoğan naye alibainisha lengo lake la kutaka kuondoa makundi ya kigaidi kama vile DAESH na PKK katika kanda hiyo, na kusisitiza umuhimu wa operesheni za Mosul katika suala hilo.
Viongozi hao wawili pia waliarifu kwamba kundi la kigaidi la PKK halipaswi kuruhusiwa kuendeshwa harakati zake katika maeneo ya kaskazini mwa Iraq.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment