Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake wakitoka katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na DRC wakitia saini mkataba wa makubaliano ya pamoja (MOU) wa utafutaji na uendelezaji wa mafuta katika eneo la upande wa magharibi mwa afrika Mashariki hususan katika ziwa Tanganyika
Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na DRC wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkataba wamakubaliano ya pamoja (MOU) wa utafutaji na uendelezaji wa mafuta katika eneo la upande wa magharibi mwa afrika Mashariki hususan katika ziwa Tanganyika
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila akiongea na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila akiongea na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila akiongea na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Wajumbe wakimpigia makofi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila wakati akiongea na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo
Wajumbe wakimpigia makofi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake wakitoka katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila na ujumbe wake katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe Joseph kabila na ujumbe wake katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
====================================
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wamefanya
mazungumzo rasmi Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na wananchi
kupitia vyombo vya habari ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza
na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi
mbili marafiki na majirani.
Katika Mazungumzo
hayo Rais John Pombe Magufuli amemuhakikishia Rais Joseph Kabila Kabange kuwa
Serikali ya Tanzania imechukua hatua kadhaa za kuimarisha huduma katika bandari
ya Dar es Salaam na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kubaki vitatu ili
nchi ya Kongo na nchi nyingine za kusini na magharibi mwa Tanzania ziitumie
bandari hiyo bila vikwazo.
Dkt. Magufuli
amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuhakikisha uchumi wake unakua kwa
asilimia 7.2 na kwamba kutokana na hali hiyo anawakaribisha wafanyabiashara wa
Kongo kuja kuwekeza nchini Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kwenda
kuwekeza nchini Kongo.
"Mhe. Rais
Joseph Kabila Kabange takwimu zinaonesha nchi zetu zinafanya biashara kubwa
kwani katika mwaka 2009 tulifanya biashara iliyofikia Shilingi Bilioni 23.1 na
imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka na hivi sasa tunafanya biashara yenye thamani
ya shilingi Bilioni 393.6 kwa mwaka.
"Mimi
ningependa kuona sisi ndugu na majirani tunafanya biashara zaidi,
wafanyabiashara wa Kongo waje Tanzania kuwekeza na Serikali yangu itawaunga
mkono" amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais
Magufuli amezungumzia mikakati ya kuimarisha mawasiliano ya barabara na ujenzi
wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard
Gauge) ambapo Tanzania imetenga Shilingi Trilioni 1 kwa ajili ya kuanza
ujenzi huo na kwamba hatua hiyo itarahisisha zaidi usafirishaji wa mizigo ya
kwenda na kutoka Kongo kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Kuhusu mradi wa
ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya
Tanga nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema ni matarajio kuwa Kongo ambayo pia
imegundua mafuta katika ziwa Albert itatumia bomba hilo kama ambavyo Tanzania
pia inatarajia kulitumia kufuatia tafiti kuonesha uwepo wa mafuta katika maeneo
ya ziwa Eyasi na Ziwa Tanganyika.
Kwa Upande wake
Rais Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe. Jospeh Kabila Kabange amemshukuru
Rais Magufuli kwa mwaliko huu wa ziara ya kiserikali na amemhakikishia kuwa
Kongo itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na Tanzania kwa kuwa nchi
hizi ni majirani na ndugu tangu enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Mhe. Kabila
amesema Kongo inatambua umuhimu wa kushirikiana na Tanzania katika biashara na
uwekezaji na kwamba amefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Tanzania
imezichukua kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam ambayo ni tegemeo
kwa usafirishaji wa mizigo ya Kongo Mashariki na sehemu nyingine za nchi hiyo.
Ameahidi kuwa
pamoja na kuwahasisha wafanyabishara wa Kongo kuitumia bandari ya Dar es Salaam,
Serikali yake itachukua hatua za kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa na
wafanyabiashara dhidi ya maafisa wa forodha wa Kongo waliopo hapa nchini.
Rais Kabila
amezungumzia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini
Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania akisema nchi yake pia imeamua
kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta yake iliyoyagundua katika ziwa Albert
upande wa Kongo na pia juhudi zinazoendelea kupata mafuta katika ziwa
Tanganyika na amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo ushirikiano ni muhimu.
Kuhusu hali ya
usalama nchini Kongo, Rais Kabila amesema kwa asilimia 97 nchi hiyo ina usalama
na kwamba ni maeneo machache tu ya mashariki mwa Kongo ndiko kuna vikundi
vinavyoendesha vurugu.
"Mhe. Rais
Magufuli hivi karibuni tutaanza mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini
Kongo, na lengo letu ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani kabla, wakati na
baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Desemba ama baada ya mwezi
Desemba" amesema Rais Kabila.
Mhe. Rais Kabila
amekubali kuupokea ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Tanzania,
Angola na Msumbiji ambao Mwenyekiti wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC - Organ Trioka) Rais John Pombe
Magufuli ataituma hivi karibuni kwa ajili kufuatilia hali ilivyo nchini Kongo.
Baada ya
mazungumzo rasmi na kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, Rais
Kabila anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari (TPA) lililopo kando ya Bandari ya Dar es Salaam na jioni atashiriki
dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.
0 comments:
Post a Comment