Dar es Salaam.Wakati
juhudi zikiwa zinaendelea kufanywa na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam
ya kuona namna gani ambavyo kijana Said Mrisho anaweza kurudi kwenye
hali yake ya kawaida ili aweze kuona baada ya kutobolewa macho na kijana
mmoja aliyetambuliwa kwa majina ya Salum Henjewele maarufu kama
(Scopion) limeonekana kugonga mwamba kufuatia majibu ya madaktari katika
hospitali ya Muhimbili kusema kuwa hakuna uwezekano wa kijana hyo kuona
tena.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekuwa bega kwa
bega na familia ya Bwana.Saidi baada ya kupata taarifa za kujeruhiwa kwa
kutobolewa macho maeneo ya Buguruni akifanya mahitaji mbalimbali ya mlo
wa siku alipotoka kazini, taarifa za mkasa wake ziliibuliwa na kituo
cha Clouds Fm kupitia kipindi cha leo Tena.
Mapema leo Mkuu wa Mkoa
Paul Makonda amezungumza na waandishi wa habari kuelezea hatua
iliyofikiwa hadi hivi sasa juu ya matibabu ya Saidi iliyokuwa chini ya
Madaktari bingwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ya kuhakikisha
kwamba kama kuna uwezekano wa kijana huyo kuona basi Serikali ya mkoa
itasimamia matibabu yake mpaka apone, lakini uchunguzi wa wataalam hao
umesema haiwezekani kijana huyo kuona kama mwanzo kwa kuwa System nzima
imeharibiwa.
Licha ya ripoti ya Madaktari bingwa kuonesha kuwa Ndugu saidi hawezi kuona tena bado serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ipo bega kwa bega na Saidi ili kuhakikisha kwamba anakuwa sawa licha ya kuwa hatoona itampatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake.
-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira.
-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake.
Vile vile Serikali ya Mkoa wa DSM imeahidi kuwa itatoa kiasi cha Shilingi Milioni kumi kama sehemu ya Mtaji kabla ya kupatwa na ulemavu kwani alikuwa kinyozi hivyo itasaidia biashara yake hiyo ya saloon, ambapo mdogo wake saidi atakuwa msaada wa kuhakikisha anaendeleza saloon hiyo kwa kiasi kitakacho tolewa na Serikali ya mkoa kutokana kuwa alikuwa akifanya kazi na kaka yake hivyo itakuwa rahisi.
Mama mzazi wa Saidi ndugu jamaa na Marafiki na wanahabari wameonekana kuwa na simanzi kubwa kutokana na majibu ya Daktari yakuwa Ndugu Said hatoweza kuona, ambapo mama mzazi alionekana kulia kwa uchungu mnoo kwa jinsi akimuangalia mwanaye ikiwa yeye ndio alikuwa msada katika familia hiyo.
Aidha kutokana na tukio hilo Serikali ya mkoa na Jeshi la polisi lilifanikiwa kumtia mbaroni Mtuhumiwa aliye mtoboa macho Saidi, Bwana Salum Henjewele maarufu kama (Scopion).
Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani akidaiwa kumtoboa macho, Said Mrisho maarufu kama Baba D, anafahamika kwa jina la Salum Henjewele maarufu kama Scopion ni msanii wa maigizo ya filamu na tamthilia imebainika na kwamba alishawahi kushinda mill 20 kwenye shindano la Dume Challenge 2012 pamoja na mkataba wa kuwa balozi wa mipira ya kiume ya maarufu ‘Dume’.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania siku za hivi karibuni lilisema baadhi ya watu aliowahi kufanya nao kazi walisema kuwa Scopion aliwahi kushiriki kwenye tamthilia ya Red Apple, Mirrosos na Thilipina ambayo inaendelea kukamilishwa na kuandaliwa na Chuzi Kihangala maarufu kama Mr.Chuzi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment