Image
Image

Serikali yakanusha kuwepo uhaba wa dawa nchini.

Serikali imekanusha taarifa zilizoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi pamoja na mitandao ya kijami kwamba bohari kuu ya dawa na vituo kadhaa vya afya nchini vinakabiliwa na uhaba wa dawa nakusema kuwa  taarifa hizo si sahihi na zinalenga kupotosha umma na kuwatia wasiwasi usio wa lazima wananchi.
“Dawa zote muhimu kwa binadamu  zinapatikana kwenye bohari kuu ya dawa kwa masaa 24 kinyume na watu na  Taasisi zisizo za kiserikali kusambaza maneno kuwa MSD imeishiwa dawa  kitendo ambacho sio cha kweli dawa zipo na zinasambazwa kwenye vituo vyote vya afya” Alisema Mhe. Ummy. 
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambapo amesema kwamba hali ya dawa nchini ni nzuri kutokana na dawa zote muhimu kuwepo katika maghala ya  dawa huku dawa nyingine zikiendelea kupatikana kwa kuagizwa kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Aidha Ummy amesema kuwa ili  kutekeleza mpango wa sera ya afya ya Serikali ya tano ,jumla ya shilingi bilioni 251 zimetengwa ili kuweza kuhakikisha dawa za binadamu  zinapatikana kila wakati pindi zinapohitajika kutoka MSD ili kutoa  huduma bora kwa watanzania. 
Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania. 
Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2, chanjo za Pepopunda dozi milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.
“Tulikuwa na tatizo la chanjo kama wiki nne zilizopita lakini 
tumejitahidi na tumeweza kuleta chanjo zote muhimu pamoja na kuagiza 
chanjo za surua ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuhakikisha 
chanjo zinapatikana kwa wingi nchini” alisisitiza Waziri huyo. 
Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kununua na kufanya uzalishaji wa dawa katika viwanda vya ndani ili kuweza kuchangia uchumi wa viwanda vya  ndani ili tufikie uchumi wa kati. 
Waziri Ummy aliwataka  Wakurugenzi wa Vituo vya Afya pamoja na Waratibu wa Afya wa Wilaya kuagiza dawa MSD mapema bila ya kusubiri ziishe kabisa kwenye vituo  vyao ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment