Image
Image

Uongozi wa Muhimbili wasema haujamkataza mgonjwa kutoka hospitali kwa kukosa fedha.


KUHUSU MGONJWA WA SARATANI KULIPISHWA FEDHA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unapenda kuutarifu Umma kwamba haijamzuia Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kutoka hospitalini kwa madai ya kushindwa kulipa pesa za matibabu kama ilivyoandikwa na Gazeti la Jambo Leo lenye namba ISSN 7826 No 2589, hivyo taarifa hizo si za kweli.
Katika ukurasa wa mbele, gazeti hilo limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kinachosema “Mgonjwa saratani azuiwa Muhimbili miezi miwili ni baada ya kushindwa kulipa deni la Sh. 330,000”.
Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kwa mara ya kwanza alilazwa Muhimbili Agosti 29, 2016  akitokea mkoani Morogoro na kuruhusiwa Septemba 10, 2016  na  Septemba 23, 2016  alilazwa tena na kuruhusiwa Septemba 24, 2016.
Baada ya vipimo vya awali kufanyika Septemba 29, 2016 alilazwa tena na kufanyiwa  upasuaji Septemba 30, 2016 na kuruhusiwa Oktoba 04, 2016 baada ya taratibu za matibabu kukamilika.
 Mgonjwa  aliingizwa kwenye utaratibu wa msamaha na kuchangia Shilingi 70,000 tu, kati  ya Shilingi 400,142.33. Hivyo si kweli kwamba mgonjwa alilipa Shilinngi 380,000 kama ilivyoandikwa na gazeti hilo.
Kuhusu tiba ya mionzi, Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri amefanyiwa vipimo vingine hivyo atatakiwa kurejea baada ya wiki tatu kwa ajili ya majibu na si kweli kwamba Muhimbili imezuia uhamisho wake kwenda Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa ajili ya tiba hiyo.
Imetolewa na;
Uongozi wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili
Oktoba  10, 2016.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment