Image
Image

Siku ya pili ya uhamishaji wa wakimbizi kutoka kwenye kambi ya Calais Ufaransa yazua utata

Harakati za uhamishaji wa wakimbizi kutoka kwenye kambi ya Calais nchini Ufaransa zinaarifiwa kuendelea ambapo hadi kufikia sasa, wakimbizi 4,014 wameweza kuhamishwa.Hali imeonekana kuwa na mvutano tangu siku ya kwanza huku wakimbizi wengi wakilazimika kusubirishwa kwenye foleni ndefu kwa masaa mengi.
Mara kwa mara ghasia zimeripotiwa kutokea miongoni mwa wakimbizi hao huku maafisa wa polisi wakishika doria kudhibiti hali ya usalama.
Wakimbizi wengi wa umri usiozidi miaka 18 wanaarifiwa kuulizwa maswali yasiyokuwa na msingi wakati wa kuhojiwa na kutakiwa kuthibitisha endapo walifahamu lugha ya Kifaransa au Kiingereza na kama wanao jamaa zao Uingereza.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa, jumla ya watu  1,264 wakiwemo watoto 372 walihamishwa na kuwekwa kwenye vituo vya hifadhi nchini humo.
Watoto 217 pia wameweza kuhamishiwa Uingereza tangu tarehe 17 Oktoba.
Kwa upande mwingine, kumezuka utata kuhusiana na mabasi ya usafiri yanayotumika kwenye shughuli ya uhamishaji wa wakimbizi.
Viti vya mabasi hayo vimeonekana kufunikwa kwa mifuko ya plastiki ili kuzuia uchafu na ueneaji wa maradhi.
Meya wa Calais Natacha Bouchart alitoa maelezo na kuarifu kuchukuwa hatua hiyo kama tahadhari baada ya kufanya mazungumzo na kampuni za mabasi ya usafiri.
Hali hiyo ilizua utata katika mitandao ya jamii ambapo wengi walitambua tukio hilo kuwa la udhalilishaji wa wakimbizi.
Maafisa wa polisi pia walionekana kuziba nyuso zao, kuvaa glovu za plastiki mikononi na kufunika viatu vyao vya mifuko.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment