WAKATI Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akitoa onyo na kuwataka wale
wote wanaotumia vibaya jina la ofisi ya Msajili ili kuichafua ofisi
yake au kwa lengo la kukidhi hisia na matakwa yao binafsi waache kabisa
tabia hiyo, Baraza la Udhamini la Chama cha Wananchi (CUF) limesema
linafanya utaratibu wa kuzikutanisha pande mbili za uongozi wa chama
hicho kwa lengo la kumaliza mgogoro uliopo.
Kwa siku kadhaa sasa CUF imekumbwa na mgogoro wa kiuongozi kati ya
Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wake
aliyepata kujiuzulu na kurejea tena Profesa Ibrahim Lipumba.
“Tunauomba umma wa Watanzania kutambua kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa ni taasisi inayoendeshwa kwa kufuata misingi na taratibu za
sheria za nchi.
Aidha tunawaasa wadau wa habari kutoa taarifa baada ya
kujiridhisha na usahihi wa taarifa hizo, na kujikita kwenye taarifa
zinatolewa rasmi na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa badala ya
kuuaminisha umma na kuupotosha kwa makusudi,” ilieleza taarifa ya Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Monica Laurent wa Ofisi ya
Msajili.
Kwa upande wake, Baraza la Udhamini la CUF kupitia kwa Mwenyekiti wa
kikao kilichoketi wiki hii na Mjumbe wa baraza hilo, Peter Malebo
alisema mgogoro uliopo ndani ya chama hicho utamalizwa ndani ya chama
hicho baada ya kuzikutanisha pande hizo mbili.
“Tatizo lililopo ndani la CUF ni tatizo la muda mrefu na wajumbe wa
bodi ya chama hicho ndio wenye jukumu la kumaliza mgogoro huo, lakini
mbaya zaidi baadi ya wajumbe wamekuwa ndio wanachonganisha na kukuza
mgogoro huo badala ya kuumaliza,” alisema Malebo.
Aidha, Malebo alisema wanampongeza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi kwa kutolea ufafanuzi wa sakata la uongozi wa chama
hicho na kumthibitisha Profesa Lipumba kuwa ni Mwenyekiti halali wa
chama hicho kwa mujibu wa Katika ya chama chao.
Home
News
Slider
Sinto fahamu iliyopo katika siasa, Msajili wa vyama vya siasa nchini avunja ukimia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment