JAMII imetakiwa kumpa kipaumbele mtoto wa kike kwa sababu ana uwezo wa kuendelelza vizazi vijavyo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Eda Sanga, wakati akifungua mafunzo
ya usalama barabarani, sambamba na maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
kimataifa, ambapo amesema ipo haja ya mabadiliko ya mifumo ya kisheria
ambayo imekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike.
Alisema ajali za barabarani zinapotokea mtoto wa kike anaathirika kwa
kiasi kikubwa baada ya kuondokewa na wazazi wake pindi ajali inapotokea
na kumsababishia kubeba mzigo wa kutunza familia akiwa bado mdogo.
Eda alisema pia ipo haja ya kuharakisha mchakato wa kubadilisha
sheria kandamizi zikiwemo mila potofu ambazo zimekuwa zikididimiza
maendelelo ya mtoto wa kike.
“Nina imani mtoto wa kike akipewa nafasi anaweza hivyo ni lazima jamii iendane na wakati,” alisema Eda.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokubali kuingia mikataba
ya kimataifa kulinda haki za watoto, hata hivyo Sheria ya Ndoa ya mwaka
1971 bado ni kandamizi.
Naye Mratibu wa Programu ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones
John alisema maadhimisho ya siku ya mtoto kimataifa yanawakumbusha
wanaharakati kupigania haki bora ikiwemo kuikumbusha serikali kubadili
vikwazo vinavyochangia ukiukwaji haki za watoto.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment