Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo 25-Oct-2016 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Sandeep Arya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesema mahusiano kati ya Tanzania na India yamesaidia
kunufaisha wananchi wa nchini mbili hasa katika masuala ya
kibiashara,miradi ya maendeleo na hivyo mahusiano hayo ni muhimu
yakaendelezwa na kudumishwa.
Makamu
wa Rais katika mazungumzo na balozi huyo wa India hapa nchini Sandeep
Arya pia ameiomba serikali kuisaidia Tanzania katika mpango utakaosaidia
wakulima kupata taarifa mbalimbali zinazohusu kilimo na masoko ya
bidhaa zao kupitia simu za mkononi ili kuondoa usumbufu mkubwa wanaopata
wakulima kwa sasa hasa kuhusu masoko.
Kwa
upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya
amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan serikali yake itakuwa bega kwa bega na Tanzania katika
kuhakikisha wananchi wa pande Mbili wananufaika na mahusiano yaliyopo.
Balozi
Sandeep Arya amesisitiza kuwa serikali ya India itaendelea kuisaidia
Tanzania katika uimarishaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano
pamoja na miradi ya maendeleo na uimarishaji wa shughuli za kiuchumi.
Wakati huo huo,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sudan nchini Tanzania
Mahgoub Sharfi mazungumzo yaliyolenga pamoja na mambo mengine kuhusu
namna ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Sudan.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam.
25-Oct- 2016.
0 comments:
Post a Comment