Chuo
cha utangazaji na uandishi wa habari Time School of Journalism (TSJ)
kilichopo ilala Dar es Salaam kimepatwa na msiba wa moja ya Mkurugenzi
wake Mr. Zidadu ambaye amefariki dunia.
Taarifa ambazo
zimetufikia hazijabaini kuwa nini kilimfika na kusababisha umauti wake
lakini taarifa zimeeleza kuwa tumempoteza na hatunaye tena
duniani,Taarifa kamili tutawajuza.
Taarifa za kifo chake simeelezwa
na moja ya Mwalimu chuoni hapo ambaye hakuweza kusema nini
kilisababisha kwa kuwa si msemaji lakini alikiri kupokea taarifa hizo za
msiba ambazo ni za kweli zikieleza kuwa Mr.Zidadu amefariki katika Hospitali ya Mwananyamala na kusema nipigo pia katika chuo kwa kupoteza
mkurugenzi wake wa siku nyingi na Mwanzilishi wa Chuo cha TSJ ambacho
kimefua wana habari mbali mbali na kujipatia ujuzi wa mambo lukuki,
alisema daima watamkumbuka.
Taratibu za Msiba zinaendelea kufanyika
ambapo Msiba inaelezwa kuwa kwaq watakao kwenda kuhudhuria safari ya
mwisho ya Mzee wetu Marehemu Zidadu nikwamba Ukifika Geti La Mwananyamala Hospitali Utaona Maturubai Upande Wa Pili Au Ukuta Wa Ofisi Za Dawasco Mwananyamala Mazishi Kuanzia Saa 7 Hadi 9 Karibu Na Msikiti Wa Magomeni leo.
Wanafunzi
waliosoma TSJ Mnaombwa kufika ikibidi ili kumpumzisha mzee wetu huyu
Zidadu,ikumbukwe tu kwamba TSJ imeitwa TSJ kutokana na mchango wake na
mashirikiano na wakurugenzi waliobaki, ambapo asilimia 80% ya
watangazaji na waandishi ni wazi kuwa nichimbuko la TSJ walioko katika
Media mbalimbali Dar na Mikoa mingine ama nje ya Tanzania walipata
kusoma chuoni hapo.
Uongozi wa Tambarare Halisi unatoa Pole kwa familia nzima ya marehemu katika kipindsi hiki kigumu,na Uongozi mzima wa Chuo cha TSJ ilala Sharif Shamba JIJINI Dar es Salaam.
Home
News
Slider
Tanzia:Mkurugenzi wa chuo cha (TSJ) Mr.Zidadu afariki Dunia,Taarifa kamili ipo hapa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment