Katika ziara hiyo aliyoifanya Oktoba 3, 2016 Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu inayohitajika.
Katika
ziara hiyo Waziri mkuu ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka
ya Ustawishaji wa Makao Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa
miundombinu ya biashara kama masoko na hoteli na viwanda na
tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya kutosha.
Wakati huo huo Waziri
Mkuu amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo
ya ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na
kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.
Aidha amebainisha kuwa muwekezaji
atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan
Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.
“Tumekaribisha
pia wawekezaji wa ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na
uzalishaji ni mkubwa Kanda ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara,
Singida na mikoa ya jirani ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na
fursa hizo,” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi
Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo
ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297,
Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370.
0 comments:
Post a Comment