Mgombea
urais Marekani wa chama cha Republican Donald Trump amekataa kuahidi
kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala wa mwisho
wa urais dhidi ya Hillary Clinton.
"Nitakuambia wakati huo"
alimwambia muendesha mjadala Chris Wallace. Kwa siku kadhaa amedai kuwa
kuna 'udanganyifu' katika uchaguzi huo.
Mjadala huo wa televisheni Las Vegas uliendeleza uhasama katika kampeni huku Trump akimuita Bo Clinton "mwanamke muovu".
Kura
za kutafuta maoni zinaonyesha Trump poteza umaarufu katika majimbo
makuu baada ya kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.
Mjadala huo wa mwisho wa umefanyika wiki tatu kabla ya siku ya uchaguzi Novemba 8.
Wagombea
hao walikataa kusalimiana kwa mikono kabla na baada ya majibizano hayo
ya kisiasa, hatua iliyofungua kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa
mjadala wa kelele na kukatizana kauli.
Trump alitoa ahadi kwa
wanachama wa Republican kuwateua majaji wa mahakama ya juu zaidi
wanaoegemea 'mrengo wa kihafidhina' watakaogeuza sheria kuu
inayohalalisha uavyaji mimba Marekani na kulinda haki za kumiliki
bunduki.
Alisisitiza ahadi yake ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji ambao hawakusajiliwa na kudhibiti mipaka ya Marekani.
Wakati
huo huo, Bi Clinton ametangaza wazi kuwa atawatetea wapenzi wa jinsia
moja, atalinda haki za kuavya mimba, atalenga kuinusha watu wa kipato
cha wastani na kushinikiza kulipwa sawa kwa wanawake.
"Serikali haina shughuli yoyote katika maamuzi wanayofanya wanawake," alisema.
Katika
mojawapo ya nyakati zilizokuwa na mvuto, Trump alikataa mara mbili
kusema iwapo atakubali matokeo ya uchaguzi, hatua iliyobadili utamaduni
wa muda mrefu wa wagombea wanaoshindwa kukubali matokeo baadaya kura
kuhesabiwa.
Majibu ya Trump yamezusha shutuma kali kutoka kwa seneta
wa Republican Lindsey Graham, aliyesema mgombea huyo "hawajibi ipasavyo
kwa chama chake na taifa kwa kuendelea kuashiria kuwa anafanyiwa
udanganyifu katika uchaguzi ujao," kwa mujibu wa taarifa.
Kauli nyingine kuu katika mjadala katika chuo kikuu cha Nevada ni :
Bi Clinton anasema Putin anataka Trump achaguliwe kwasababu anataka kinyago awe rais wa Marekani.
"Tuna watu wabaya na tuta watoa," amesema Trump, aliposhinikiza ahadi yake ya kujenga ukuta mpakani.
Bi Clinton amesema ataidhinisha mpango mkubwa wa ajira kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.
Trump ameashiria bi Clinto na rais Barack Obama walipanga ghasia katika mkutano wake wa kisiasa Chicago mapema mwaka huu.
"Hilo ni jambo la kuogofya," Clinton akajibu kwa ukali.
"Anaponda
na kudharau demokrasia yetu. Na mimi kivyangu, nimeshangazwa kuwa mtu
ambaye ni mgombea mteule wa mojawapo wa vyama viwili vikuu anaweza
kuchukua msimamo wa aina hiyo."
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment