SODA, chumvi vinaongoza kwa kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwamo shinikizo la damu, MTANZANIA limeelezwa.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania
unaonyesha asilimia 27 ya Watanzania wamebainika kuwa na shinikizo la
damu.
Akizungumza na Jukwaa la Waandishi wa Habari na Wahariri wa Kupambana
na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza Tanzania (TJNCDF), Profesa Andrea
Swai alisema magonjwa yasiyoambukiza ndiyo yanayoongoza kwa idadi kubwa
ya vifo.
Alisema asilimia tisa ya Watanzania wote wamebainika kuwa na ugonjwa
wa kisukari huku ugonjwa wa saratani ukiongoza mara mbili ya wagonjwa
wanaopokelewa hospitalini.
“Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ndiyo yanaongoza kwa vifo na hii
inatokna na vyakula tunavyokula ikiwa ni pamoja na chumvi, soda na
chips,” alisema Profesa Swai.
Alisema ili kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza ni lazima waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema ili
kuweza kuhabarisha umma.
Alisema kila mmoja anajukumu la kupambana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza kwa kuzingatia anafanya mazoezi ya kutosha ili kuimarisha
afya ya mwili wake.
“Ifike wakati tuwe na utamaduni wa kufanya mazoezi kwa ajili ya
viungo vyetu hii itatusaidia kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza,”
alisema Profesa Swai.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment