MAOFISA 14 utumishi wa Halmashauri za Momba, Tunduma, Mbozi na Ileje
katika Mkoa wa Songwe wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuzalisha
watumishi hewa na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Pamaoja na kusimamishwa kazi vigogo hao, pia walikamatwa na kuwekwa rumande kwa siku nne kabla ya kutolewa kwa dhamana.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni mstaafu Chiku Galawa, akizungumza kwa
njia ya simu akiwa safarini, alithibitisha watendaji hao kusimamishwa
kazi na kwamba hatua hizo zimechukuliwa na mamlaka zao za nidhamu.
“Hao wote ukiacha Wilaya moja tu ya Songwe ambayo masuala yao
yatashughulikiwa katika Wilaya ya Chunya kwa kuwa hayo yalifanyika kabla
ya kugawanywa, lakini wote waliobaki wamechukuliwa hatua hizo na
mamlaka zao za nidhamu ambazo ni Wakurugenzi Watendaji, ili kupisha
uchunguzi wa tuhuma zao,” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Galawa alisema baada ya uchunguzi kukamilika hatua mbalimbali
zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo baadhi yao kufikishwa mahakamani kwa
kuwa baadhi ya makosa yaliyoainishwa na mamlaka zilizochukua hatua
yanaonekana ni ya jinai.
“Kuhusu hilo la takwimu kwamba ni kiasi gani cha hasara ya fedha
waliyoisababisha hasara serikali niombe tu kuwa sina uhakika maana niko
nje ya ofisi, nisije kukupa kitu kisicho halisi, halafu baadae
mkanigeuka tena,” alisisitiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Nyange
Mathias alithibitisha jeshi hilo kuwashikilia watumishi hao na
wanaendelea na uchunguzi dhidi ya watumishi hao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment