Image
Image

Uturuki yagawana pointi na Ukrein baada ya kutoka sare ya 2-2 kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia la FIFA 2018

Timu ya taifa ya Uturuki iliikaribisha Ukrein kwenye mechi yao ya pili ya makundi ya kuwania kufuzu mashindano ya kombe la dunia la FIFA 2018.Mechi hiyo ilichezwa katika uga wa Torku Arena ulioko mjini Konya nchini Uturuki.
Timu ya taifa ya Uturuki ilianza vibaya mechi hiyo na kumaliza kipindi cha kwanza 2-1 baada ya kufungwa na Ukrein. 
Lakini katika kipindi cha pili, Uturuki ilicheza vyema zaidi na kufanikiwa kumaliza mechi hiyo kwa sare ya 2-2.
Magoli ya Uturuki yalifungwa na Ozan Tufan na  Hakan Çalhanoğlu huku Ukrein ikipata magoli yake kupitia wachezaji Andriy Yarmolenko na  Artem Kravets.
Mwenyekiti wa zamani wa AKP na waziri mkuu wa zamani Ahmet Davutoglu pamoja na rais wa TFF Yıldırım Demirören walitazama mechi hiyo uwanjani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment