Askari mmoja ameripotiwa kufariki baada ya kushambuliwa na
bomu lililotegwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la PKK katika mkoa wa
Van.Gavana wa mkoa wa Van amefahamisha kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na wanamgambo wa PKK.
Van ni mkoa unaopatikana mashariki mwa Uturuki ambapo mara nyingi wanamgambo wa PKK huendesha mahambulizi yao.
Jeshi la Uturuki limeanzisha operesheni baada ya tukio hilo ili kuwatia mbaroni walohusika na shambulizi hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment